Manchester United imeweka kipaumbele katika usajili wa nahodha wa Aston Villa Jack Grealish, 24, msimu huu lakina inaweza kubadili mipango yake ikiwa mchezaji Kai Havertz wa klabu ya Bayer Leverkusen atapatikana. (Manchester Evening News)
Hata hivyo, Bayern Munich inaamini kwamba inakaribia kuzipiku vilabu vingine ikiwemo United katika usajili wa mchezaji huyo – United imekuwa ikiongoza kwa vilabu vilivyoonesha nia ya kumsajili mshambuliaji Havertz, 20, kati ya vilabu vingine maarufu vya Ulaya. (Independent)
Winga wa PSG Angel di maria 32, ambaye hivi karibuni alihusishwa kujiunga na Barcelona amesema anajisikia furaha kuwepo hapo na hawezi kujiunga na Barcelona hata kama watahitaji sahihi ya muargentina huyo. (Goal. Com)
Leicester City haina haraka ya kumsainisha mlinzi wake Ben Chilwell 23, anayehitajika na Chelsea ikiamini kwamba kufuzu kwa msimu ujao katika Ligi ya Mabingwa kutawaweka katika nafasi nzuri ya kuendelea kuwa na mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza. (Leicester Mercury)
Mshambuliaji wa lille victor osimhen 21,amekanusha taarifa zinazoenea kuwa tayari amekubalia kujiunga na Napoli katika kipindi cha majira ya kiangazi. (Transfer market web)
Klabu ya hellas verona imeridhika na kiwango kilichoonyeshwa na mshambuliaji wake wa mkopo kutoka inter Milan Eddie salcedo 18, na kutaka kumbakisha kwa msimu ujao.(Transfer market web)
Shirikisho la soka nchini ufaransa Limesema Dirisha la usajili nchini humo kwa msimu ujao 2020/2021 litafunguliwa jumatatu June 08/2020. (Goal.com)
Wakati huohuo, Leicester, maarufu kama The Foxes, wanataka angalau £60m kwa mchezaji wao Ben Chilwell. (Guardian)
West ham imejiunga na Arsenal katika mbio za kumuwania winga wa Iran kutoka zenit St Petersburg sardar Azmoun 25, katika majira ya kiangazi. (Eye football)
Mshambuliaji wa zamani wa Barcelona Rivaldo amesema lazima Barcelona ichague mchezaji mmoja kati ya lautaro Martinez 22, na Neymar Jr 27, Na anaamini miamba hiyo ya laliga haiwezi kuwasajili wote licha ya kuhusishwa na wachezaji hao wawili. (Evening standard)
Winga wa Manchester City Leroy Sane atasaini mkataba wa miaka mitano na Bayern Munich. Lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, 24, hatakuwa mchezaji mwenye kulipwa kiwango cha juu zaidi katika ligi ya Ujerumani. (Bild)
Everton iko tayari kumtafuta nahodha wa Paris St-Germain Thiago Silva, ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa Juni. Timu ya awali ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil, 35, AC Milan pia imeonesha nia ya kutaka kumsajili. (Le10Sport)
Upande mwengine Arsenal inapania kumsajili mlinzi wa Norwich City, Max Aarons, 20, lakini haiko tayari kulipa £30m. (Goal via Norwich Evening News)
Licha ya kufuatiliwa na kuhitajika na vilabu vya Barcelona, Arsenal pamoja na Fiorentina sasa juventus nao wamejiunga kataka timu zinazohitaji kupata sahihi ya winga wa Roma mdutchi Justin kluivert 21. (dello sport)
Manchester City imewasiliana na Barcelona kuhusu mshambuliaji Sergi Roberto. Lakini mchezaji huyo wa Uhispania, 28, ataondoka Nou Camp ikiwa tu klabu hiyo itamuarifu kwamba sasa anaweza kuhamia kwengineko. (Mundo Deportivo, in Spanish)
Kiungo wa Bayern Munich mhispania Javi Martinez 31, anamachaguo matatu kujiunga na ligi kuu marekani, Australia pamoja na nyumbani kwao Hispania baada ya mkataba wake na Bayer utakapofikia tamati msimu huu. (Sport mole)
Inter Milan inaweza kufikiria uwezekano wa kumuuza mlinzi wake wakati MSlovakia Milan Skriniar, ambaye amehusishwa na Manchester City, ikiwa tu watapokea pendekezo la kumuuza mchezaji huyo kwa zaidi ya thamani ya €80m. (Tuttosport via Manchester Evening News)
Real Madrid wanataka kumsajili mshambuliaji wa Tottenham’s Hotspurs mkorea kusin Son meung – min 27, katika majira ya kiangazi. (Sport mole)
Kinda la Arsenal muingereza mwenye asili ya Nigeria Miquel Azeez 17, amesaini mkataba rasmi na Arsenal kama mchezaji wa kulipwa Azeez alijiunga na Gunners akiwa na miaka mitano na atpandishwa rasmi kwenye timu ya wakubwa kuanzia msimu ujao. (Arsenal News)
Mshambuliaji wa Chelsea Pedro Rodriguez 32, amekubaliana maslai binafsi na As Roma ili kujiunga kama free player baada ya msimu huu mkataba wake utakapomaliziaka (dream transfer)