Connect with us

Soka

Man Utd Yaizunguka Real Madrid

Klabu ya Man utd imeanzisha mazungumzo na Ajax juu ya kumsajili kiungo Donny Van De Beek kutokana na taarifa nchini Uholanzi.

Awali iliripotiwa kwamba Real Madrid imekubaliana na Ajax kiasi cha paundi milioni 44 kumsajili kiungo huyo na ilibaki kukamilisha vipimo vya afya tu lakini dili hilo mpaka sasa limesimama kufuatia matatizo ya kifedha yaliyosababishwa na Virusi vya Corona.

Man utd inataka kutumia mwanya huo kukamilisha dili hilo huku uhusiano wake mzuru na mtendaji mkuu wa Ajax Edwin Van De Sar ukichagiza dili hilo kukamilika mapema huku United ikitaraji kukamilisha dili hilo kwa bei ya chini kuliko Real Madrid.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka