Connect with us

Soka

Man Utd kukosa Varane kwa majeraha

Klabu ya Manchester United imethibitisha kuwa itamkosa beki wake wa kati Mfaransa Rafael Varane kwa wiki kadhaa kutokana na maumivu kwenye eneo la kinena wkati akiitumikia timu yake ya Taifa ya Ufaransa kwenye mchezo wa fainali wa michuano ya ligi ya Mataifa Ulaya.

Katika mchezo huo Varane aliumia kipindi cha pili na kushindwa kuendelea ambapo nafasi yake ilichukuliwa na beki wa Bayern Munich Dayot Upamecano.

Beki huyo amekuwa mhimili muhimu katika kikosi cha Man Utd tangu kusajiliwa katika dirisha lililopita akitokea Real Madrid na ametengeneza kombinesheni nzuri kati yake na nahodha wa timu hiyo Harry Maguire.

Hili ni pengo kubwa sana kwa Mashetani Wekundu kwani tayari inamkosa nahodha wake Harry Maguire kwa maumivu ya kigimbi cha mguu,hivyo kuwa na wakati mgumu kuelekea ratiba ngumu ya mwezi huu wa Oktoba.

Timu hiyo sasa itawategemea zaidi mabeki Eric Bailly na Victor Lindelof katika safu ya ulinzi pamoja na majeruhi wa muda mrefu Phil Jones aliyerejea hivi karibuni na kwa namna hiyo presha inazidi kupanda kwa kocha mkuu wa kikosi hicho Ole Gunnar Solskjaer kutokana na kukosa matokeo ya kuridhisha siku za hivi karibuni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka