Connect with us

Soka

Man city,Spurs zapeta epl

Ligi kuu ya England imeendelea tena Januari mosi kwa michezo kadhaa huku vinara Man city wakisafiri hadi London kukipiga dhidi ya washika bunduki Arsenal.

Mchezo huo wa mapema ulifanyika katika uwanja Emirates Jijini London,huku city akiondoka na ushindi muhimu wa 2-1 licha ya kutanguliwa kwa bao la Bukayo Saka dakika ya 32 ya kipindi cha kwanza.

Kipndi cha pili ziliendelea kushambuliana kwa zamu huku Man city wakijaribu kusawazisha bao hilo bila mafanikio mpaka dakika ya 55 Riyad Mahrez aklipofunga kwa penati baada ya Granit Xhaka kumchezea vibaya Benardo Silva.

Kiungo Rodrigo aliiandikia timu yake bao la ushindi dakika ya 90+3 na kiwezesha na kupata alama zote tatu za mchezo huo.Beki wa kati wa Arsenal Gabriel alipewa kadi nyekundu ambayo kwa kiasi kikubwa iliwaangusha wenzake na kuchangia kupoteza.

Matokeo mengine kwenye ligi hiyo ni kama ifuatavyo; Watford 0-1 Tottenham Hotspurs,Crystal Palace 2-3 West Ham United,huku mchezo mkubwa kwa raundi hii ya 21 utakuwa ni kati ya Chelsea dhidi ya Liverpool Jumapili jioni Stanford Bridge London.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka