Connect with us

Makala

Mamelod Sundowns Yakomaa na Feisal

Klabu ya Mamelodi Sundowns inampango wa kutuma ofa ya pili kwenda klabu ya Azam FC kwa ajili ya kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo Feisal Salum ambaye imeanza mazungumzo na klabu yake ya Azam Fc huku maslahi yakiwa kikwazo mpaka sasa.

Azam FC inahitaji kitita cha Rand Million 36 ambazo ni karibia shilingi bilioni tano za kitanzania ili imruhusu nyota huyo kuondoka Chamazi ambapo Mamelod wanamhitaji Feisal kwa ajili ya kwenda kuziba nafasi ya Gaston Sirino aliyetimka kikosini hapo.

Azam Fc inalenga kupata faida maradufu kupitia dili hilo ambapo yenyewe ilitumiza zaidi ya shilingi za kitanzania milioni mia saba kumsajili Feisal kutoka Yanga sc gharama ambazo zinajumuisha malipo ya fedha za usajili kwa Yanga kiasi cha shilingi milioni mia mbili sambamba na pesa aliyochukua mchezaji huyo kusaini mkataba wa miaka mitatu (Signing on fees).

Msimu uliopita Feisal ikiwa ni msimu wake wa kwanza Chamaza alifanikiwa kufunga jumla ya mabao 19 huku akitoa pasi saba za mabao kwa wenzake kikosini humo akisaidia klabu yake kumaliza msimu katika nafasi ya pili ya msimamo dhidi ya Yanga sc waliokua mabingwa huku pia kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi Azam Fc ikipata nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala