Connect with us

Soka

Makambo Awaita Mashabiki

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Heritier Makambo amewataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi siku ya mchezo wa hatua ya awali ya klabu bingwa dhidi ya River United utakaochezwa nchini siku ya Jumapili uwanja wa B.mkapa jijini Dar es salaam.

Mchezo huo utakofuatiwa na marudiano baada ya siku saba ni muhimu kwa Yanga sc kushinda ili kujiweka sawa kufuzu michuano hiyo na kupunguza presha kwa mashabiki baada ya timu hiyo kufungwa na timu ya Zanaco Fc katika mchezo wa siku ya kilele cha’wiki ya mwananchi kilichofanyika wiki iliyopita.

”Mashabiki mje kwa waingi siku ya jumapili tar 12,tuje kuwajaza kwa pamoja mkumbuke ninyi ni wachezaji wa 12 uwanjani.💛💚” Aliandika mshambuliaji huyo kipenzi cha mashabiki wa Yanga sc aliyejiunga akitokea Horoya Fc ya nchini Guinnea.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka