Connect with us

Soka

Lwandamina Kuirudisha Azam Fc

Kocha mpya wa klabu ya Azam Fc George Lwandamina amesema atairudisha klabu hiyo katika mbio za ligi kuu baada ya kupotea kutokana na kupata matokeo mabovu.

Kocha huyo aliyejiunga na timu hiyo wiki hii baada ya kutimuliwa kwa kocha Aristica Cioaba kutokana na kupata matokeo yasiyoridhisha pamoja na mwenendo mbaya wa timu kwa ujumla wake.

“Nilikuwa naiangalia Azam walianza vyema ligi lakini baadaye hari ikapungua na kuanza kuanguka ndio nafasi mimi nipo hapa kazi yangu kubwa itakuwa kurekebisha hilo na tuirudishe timu katika mstari.” Alisema Lwadamina ambaye ni kocha wa zamani wa klabu ya Yanga sc na Zesco United ya nchini Zambia.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka