Connect with us

Soka

Lamine Hatihati Kuwavaa Ruvu

Daktari wa Yanga SC, Shecky Mngazija amesema kuwa beki wa klabu hiyo Lamine Moro huwa hachezi akiwa na maumivu bali jambo ambalo humfanya asimalize mechi huwa ni majeraha mapya ambayo hayajagundulika kabla.

Daktari huyo mkongwe kwenye tiba za michezo nchini amsema beki huyo husumbuliwa na majeraha mara kwa mara lakini sio yale ya kujirudia rudia ” Lamine amekuwa na majeraha ya mara kwa mara na baadhi hufikiri kuwa huwa anachezeshwa na maumivu lakini si kweli ”

” ndiyo maana ukiangalia rekodi zake utagundua kuwa amekuwa na majeraha tofauti ikiwemo enka, goti, bega na hii inategemeana pia ana asili ya mwili wa mtu ”

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka