Connect with us

Soka

Kumekucha Yanga

“Jangwani kumekucha” ndio msemo unaoweza kuutumia kuelezea mishemishe za usajili zinazoendelea katika klabu hiyo yenye makao makuu Jangwani Kariakoo Dar es salaam baada ya kuendeleza vurugu za usajili ili kujihakikishia wanarejesha ufalme uliopotea klabuni hapo.

Iko hivi,Baada ya kumaliza tamasha la kuichangia klabu hiyo la Kubwa kuliko na kupata mpunga wa kutosha jana klabu hiyo imewasainisha rasmi mikataba wachezaji wapya wa klabu hiyo Mybin Kalengo na Juma Balinya ambao walitambulishwa rasmi siku ya jumamosi wakati wa Tamasha hilo la kubwa kuliko.

Balinya aliyemaliza ligi ya uganda na kuwa mfungaji bora wa ligi hiyo amesaini mkataba rasmi wa miaka miwili sawa na Kalengo ambaye ni mshambualiaji wa timu ya taifa ya vijana ya Zambia na akiichezea Zesco united ya nchini humo.

Yanga imesainisha rasmi baada ya tetesi za muda mrefu kuwa imemalizana na nyota hao,ikumbukwe timu hiyo inapambana kukamilisha usajili mapema ili kutuma majina ya wachezaji watakaoshiriki michuano ya klabu bingwa barani Afrika ambapo tarehe ya mwisho ya kukamilisha usajili huo ni juni 30 mwaka huu kwa mujibu wa Caf.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka