Connect with us

Soka

Kotei Kurudi Simba sc

Kulekea katika usajili wa dirisha dogo klabu ya Simba sc ipo mbioni kumrudisha kiungo James Kotei iliyoachana nae misimu wa 2018/2019 baada ya kocha Sven Vandebroek kupitisha usajili huo.

Inadaiwa kwamba baada ya klabu hiyo kuachana na kiungo Mbrazil Gerson Fraga aliyeumia goti klabu hiyo ipo mbioni kumsajili kiungo huyo baada ya mmoja ya viongozi wa juu wa klabu hiyo kumuonyesha kocha Sven video za kiungo huyo mkata umeme ndipo kocha alikubali usajili huo.

Kotei aliondoka klabuni hapo na kujiunga na Kaizer Chiefs ya nchini Afrika ya Kusini lakini alitemwa baada ya kukosa nafasi ndipo alipojiunga na klabu ya Slavia Mozyr ya nchini Beralus alipo mpaka sasa kwa mujiubu wa mtandao wa Wikipedia.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka