Connect with us

Soka

Kotei Huru Kuja Bongo

Klabu ya ligi kuu nchini Belarus, FC Slavia Mozyr wameachana na kiungo wa kimataifa wa Ghana, James Agyekum Kotei baada ya miezi mitano tu Kotei anaondoka kwenye Klabu hiyo kwa makubaliano ya pande zote kwani alishindwa kupata nafasi ya kuanza XI tangu ajiunge mnamo Januari 2020.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na Mazyr baada ya kuachana na miamba wa soka Afrika Kusini, Kaizer Chiefs FC kwa kukosa muda wa kucheza Nyota wa zamani wa Liberty Professional ameshindwa kuanza hata game moja kwenye Ligi Kuu ya Belarus msimu huu baada ya mechi 13 Alikuwa kwenye benchi mara tatu tu.

Kotei aliwahi kuitumikia Simba SC ya nyumbani Tanzania kabla ya kuelekea Afrika Kusini baada ya kucheza kwa mafanikio Akiwa na Mnyama, alitwaa ubingwa wa Tanzania mara mbili mfululizo na pia alifika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa ya CAF msimu wa 2018/2019.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka