Connect with us

Soka

Koffi Olomide Kutumbuiza wiki ya Mwananchi

Klabu ya Yanga sc  imezindua rasmi wiki ya mwananchi visiwani Zanzibar ambapo kilele cha tukio hilo kinatarajiwa kufanyika siku ya Jumapili Agusti 29 katika uwanja wa Mkapa jijini ambapo mwanamziki Koffi Olomide anatarajiwa kutumbuiza.

Katika kilele hicho licha ya kutambulisha mwanamziki huyo kama mtumbuizaji mkuu pia mastaa waliosajiliwa na nklabu hiyo watatambulishwa rasmi kwa mashabiki huku wakicheza mechi kwa mara ya kwanza mbele ya mashabiki hao wenye hamu ya kuwaona mastaa wapya wakiongozwa na Heritier Makambo ambaye bado yupo kinywani mwa mashabiki nchini.

Katika kuelekea kilele hicho pia siku ya Jumatano klabu hiyo itatambulisha jezi rasmi za klabu zitakazotumika katika ligi kuu pamoja na michuano ya kimataifa.

Hii ni mara ya pili kwa klabu hiyo kuandaa tamasha hilo maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa msimu mpya ambapo kwa mwaka jana Tamasha hilo lilifanikiwa kujaza sehemu kubwa ya uwanja.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka