Connect with us

Soka

Kocha Stars Ameyatimba

Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Adel Amrouche ameyatimba baada ya shirikisho la soka barani Afrika(Caf) kumfungia kutokana na kutoa kauli mbaya juu ya Shirikisho hilo wakati wa mkutano na vyombo vya habari kuelekea mchezo wa kwanza wa michuano ya Afrika dhidi ya Morocco.

Katika mkutano huo kocha huyo alilishutumu Shirikisho la soka la nchi hiyo kuwa lina nguvu kiasi cha kuamua nani achezeshe mechi husika kauli ambayo iliwakera mabosi wa Shirikisho la soka nchini humo ambao walifungua malalamiko Caf kutokana na shutuma za kocha huyo.

Kutokana na malalamiko hayo ya Shirikisho la soka nchini Morocco Caf imemfungia kocha huyo mechi nane huku akipewa nafasi ya kukata rufaa kama ana ushahidi wa tuhuma hizo ambapo akimaliza kifungo hicho tayari mkataba wake na TFF utakua umeisha rasmi.

Kamati tendaji ya TFF tayari imekutana kujadili suala hilo ambapo imemteua Hemed Moroco pamoja na Juma Mgunda kuwa makocha wa Taifa Stars mpaka Afcon itakapoisha ambapo wataiongoza Stars katika michezo miwili dhidi ya Zambia na Congo Drc huku kukiwa na uhakika kuwa TFF itaachana na kocha huyo pindi mkataba wake utakapoisha.

Katika mchezo wa kwanza Stars ilikubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Morocco hivyo ina kazi ya ziada kupata matokeo ya ushindi katika  michezo miwili ili kupata uhakika wa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya timu za Taifa barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka