Muda mfupi baada ya kutambulishwa katika klabu ya Simba sc kocha Kocha Fadlu Davids ampokutana kwa mara ya kwanza na baadhi ya viongozi wa timu hiyo akiwepo Mwenyekiti wa Klabu, Murtaza Mangungu sambamba na viongozi wengine wa bodi ya wadhamini na washauri wa klabu hiyo.
Katika kikao hicho kifupi kilichoambatana na kikao na wachezaji wote wa klabu hiyo kilichofanyika katika hoteli ya Seascape jijini Dar es salaam ambapo kocha huyo alitambulishwa rasmi kwa wachezaji sambamba na benchi lake la ufundi.
Katika kikao hicho kocha huyo mbali na Mangungu na Crecentius Magori ambaye anahusika zaidi na usajili pia kocha huyo alikutana na Tajiri wa klabu hiyo Mohammed Dewji ambaye alizungumza kuhusu namna ambavyo anatamani klabu hiyo irejee kwenye makali yake kama miaka ya nyuma huku akisisitiza kila mtu kutimiza majukumu yake.
Fadlu akiwa na wasaidizi wake Darian Wilken, Mchambuzi wa video, Mueez Kajee na Kocha wa Viungo, Riedoh Berdien waliambatana na Kocha Seleman Matola ambaye nae amepewa kazi ya kuwa msaidizi namba mbili wa kocha huyo.
Kocha huyo alipata wasaa wa kupitishwa katika mikakati na malengo mbalimbali ya timu hiyo kwa msimu ujao sambamba na kukutana na wachezaji ambao walitambulishwa kwa kila upande na viongozi wa klabu hiyo.
Fadlu mwenye uzoefu wa michuano ya kimataifa Afrika baada ya kuhudumu kama kocha msaidizi katika klabu ya Raja Athletic Club ya nchini Morocco sambamba na Orland Pirates ya Afrika ya kusini atakua na kazi ya ziada kuvunja utawala wa Yanga sc na Azam Fc ambazo nazo zimeboresha vikosi vyake zaidi na zaidi.