Connect with us

Soka

Kmc Hali Tete

Timu ya soka ya Kmc imeendelea kukumbana na wakati mgumu kwenye michuano inayoshiriki msimu huu baada ya kutolewa na timu ya As kigali kwenye kombe la shirikisho barani Afrika na jana pia ipoteza mchezo wa kwanza wa ligi kuu baada ya kufungwa na Azam Fc kwa 1-0.

Bao la Azam lilipatikana dakika ya 14 likufungwa na Idd Selemani “Nado” ambapo bao hilo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Kmc haina budi kujipanga zaidi msimu huu hasa baada ya kuondokewa na nyota wake kadhaa akiwemo Emmanuel Mvuyekure aliyejiunga na Azam fc huku Ally Ally akienda Yanga na kocha Ettiene Ndayiragije akijiunga na Azam fc,Kmc sasa inafundishwa na Jackson Mayanja.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka