Klabu ya Yanga sc imeitambulisha siku ya Jumamosi Februari 24 kuwa itakua siku ya mchezaji Pacome Zouzou ambapo kutakua na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Cr Belouzdad utakaofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.
Katika kuendeleza hamasa ya mchezo huo ambao utakua maalumu kwa ajili ya staa huyo kama ilivyoutaratibu wa Idara ya habari ya klabu hiyo ambapo awali iliwahi kuzibatiza mechi hizo majina ya Ibrahim Hamad na Max Nzengeli ambapo zilileta matokeo chanya.
Meneja wa idara hiyo Ali Kamwe amesema kuwa sasa utaratibu huo tayari umepitisha na kocha Miguel Gamondi baada ya kuona kuwa inaongeza morali kwa kikosi ambapo mashabiki wanatarajiwa kupaka rangi nyeupe kwenye nywele ama ndevu ili kunogesha siku hiyo.
“GSM wameandaa Fan zone (sehemu ya mashabiki) ambapo watatoa zawadi kwa shabiki ambaye atatokelezea kitalaam zaidi siku ya Pacome Day, Sasa kazi kwenu kuhakikisha mnatokelezea kitaalamu zaidi, kimsingi ni siku ya kupendeza zaidi. Vunja kabati, jichore halafu GSM atakupatia zawadi.” Ally Kamwe Meneja Habari na Mawasiliano Young Africans SC
Kamwe pia aliendelea kusema kuwa “Tulianza na mtoko wa Max, Aziz Ki, Bacca na GSM, Mchezo wetu wa awali na CR Belouizidad wengi tulifurahishwa na namna ambavyo timu ilicheza lakini tukahuzunishwa na matokeo. Mchezo huu tunakwenda na agenda kadhaa, kushinda na kulipa deni la magoli matatu”.
“Uongozi na benchi la ufundi tumekubaliana kama taasisi Jumamosi ikawe Pacome Day, ukisema Pacome Day mwisho unamalizia Kitaalamu zaidi, unaweza kupaka rangi kichwani au kwenye ndevu. Kama huwezi kupaka rangi basi unaweza kujichora chochote na wanawake wanaweza kupaka kucha rangi.” Ally Kamwe Meneja Habari na Mawasiliano Young Africans SC
Yanga sc mpaka sasa ina alama 5 katika msimamo wa kundi D sambamba na Al ahly ambapo mshindi wa mchezo huo moja kwa moja atafufua matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi za klabu barani Afrika.