Mshambuliaji wa klabu ya Asec Mimosas ya nchini Ivory Coast Karamoko Sankara amejiunga na klabu ya Wolfsberger AC inayoshiriki Ligi Kuu Austria almaarufu ‘Bundesliga’ na kuzima tetesi kuwa anakaribia kujiunga na Yanga sc ya nchini Tanzania.
Taarifa ya Asec Mimosas kupitia mitandao ya kijamii imebainisha kuwa kinara huyo wa magoli kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu amesaini mkataba wa miaka mitatu na miamba hiyo ya Austria ambayo inakamata nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Ujerumani ‘Bundesliga’.
Sankara anaungana na mshambuliaji wa zamani wa Asec Mimosas, Karim Konate ambaye pia anachezea Bundesliga kunako klabu ya RB Salzburg huku mchezaji mwenzao waliyekua naye kikosini wakiunda kikosi hatari Stephane Aziz Ki akiwa Yanga sc.
Taarifa ya klabu ya Wolfsberger AC imesema kupitia mitandao yake ya kijamii inasomeka kuwa “Mshambuliaji mpya wa Wolves. RZ Pellets WAC inatangaza kumsajili mshambuliaji chipukizi Sankara Karamoko.”
Karamoko amekua akihusishwa na klabu ya Yanga sc ambayo tayari mpaka sasa imefanya biashara na Asec Mimosas ya wachezaji watatu Stephane Aziz Ki,Pacome Zouzou na Yao Kouasi huku ikisemekana kuwa klabu hiyo ilikua na mpango wa kumsaini Karamoko wakati wa dirisha kubwa kuziba pengo la Mayele.