Connect with us

Soka

Kanoute,Kibu Fresh Simba sc

Mastaa wa klabu ya Simba sc waliokua na majeraha tayari wamerejea kikosini humo kuendelea na maandalizi ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Asec Mimosa ya Ivory Coast siku Novemba 25 mwaka huu.

Mastaa waliokua majeruhi klabuni humo ni pamoja na Sadio Kanoute na mshambuliaji Kibu Denis,Aubin Kramo na Israel Mwenda ambao mpaka sasa ni Aubin Kramo pekee ambaye hajarejea kikosini huku wengine wakiwa tayari wamejea na wapo mazoezini na timu.

“Kikosi kipo mazoezini kuanzia siku ya Jumatatu. Mazoezi yanawahusu wachezaji wote ambao hawana majukumu ya timu za taifa. Ambao wapo kwenye timu za taifa watajiunga na wenzao wakitoka huko. Kikosi bado kipo chini ya Kocha Seleman Matola na Dani Cadena. Uongozi unaendelea na jitihada za kutafuta kocha mpya, mchakato utakamilika muda si mrefu”.Alisema Ahmed Ally meneja habari na mawasiliano wa timu hiyo.

“Kuhusu majeruhi Kibu tayari amerudi, Kanoute anaendelea vizuri, Isra Mwenda tayari amerudi mazoezini na Kramo bado anaendelea kuuguza jeraha. Akipona atarudi kutumikia klabu”.Alimalizia kusema Ahmed Ally

Simba sc iko kambini chini ya kocha wa muda Dani Cadena ikijiandaa na michuano hiyo ya hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika huku uongozi w atimu hiyo ukiwa katika harakati za kutafuta kocha mkuu kuchukua nafasi ya Roberto Oliveira “Robertinho”.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka