Kiungo Sadio Kanoute hatokua sehemu ya kikosi cha Simba sc kwa msimu ujao baada ya mabosi wa klabu ya Simba sc na mchezaji huyo kukubaliana kuachana baada ya mkataba wa mchezaji huyo kufikia tamati na mazungumzo ya mkataba mpya kushindwa kufikia muafaka.
Kanaoute Raia wa Mali anaondika klabuni hapo baada ya kuhudumu kwa miaka mitatu tangu alipojiunga na klabu hiyo msimu wa 2021 akitokea klabu ya Al ahly Benghazi ya nchini Libya ambapo punde tu baada ya kusajili alifanikiwa kupata namba kikosi cha kwanza mara kwa mara.
Kuondoka kwa staa huyo ni muendelezo wa maboresho ya kikosi hicho yanayofanywa na mabosi wa klabu hiyo kusajili mastaa wapya wa ndani na nje ya nchi baada ya kutofanya vizuri kwa takribani misimu mitatu ya ligi kuu bila kubeba taji lolote la maana.
“Kanoute alijiunga nasi msimu wa 2021/22 kutoka klabu ya Al Ahly Benghazi ya Libya kwa miaka mitatu ambayo tumekuwa na uhusiano mzuri baina yetu.Ilisomeka taarifa kutoka mtandao wa kijamii unaomilikiwa na klabu hiyo.
“Mkataba wa Kanoute umemalizika rasmi na baada ya mazungumzo ya pande mbili tumekubalina kutokuwa pamoja”.Ilimazika kusomeka taarifa hiyo
Mpaka sasa klabu ya Simba sc imeajiri benchi jipya la ufundi sambamba na kutema wachezaji takribani 19 wa ndani na nje ya nchi huku mpaka sasa mastaa 12 wapya wakiwa wamesajili kuitumikia timu hiyo.