Connect with us

Soka

InterMilan Wamkomalia Martinez

Lautaro Martinez ataondoka Inter Milan pale tu thamani yake iliyopo kwenye mkataba ( Buy-out clause ) italipwa ya kiasi cha Pauni Milioni 99.7 , amesema Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo , Piero Ausilio .

Straika huyo wa kimataifa wa Argentina ni kipaumbele namba moja cha Barcelona katika dirisha la usajili na mwezi uliopita waliwapa Inter ofa ya wachezaji katika dili la kubadilishana wachezaji .

Ausilio amethibitisha hayo mazungumzo yalifanyika na hiyo ofa ilifika kwao na kusema Barca ndio klabu iliyoonesha nia kubwa ya kumsajili Martinez lakini amesema Inter hawana nia ya kubadilisha wachezaji kama Samuel Umtiti na Nelson Semedo .

Cc.George Ambagile

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka