Connect with us

Soka

Inonga Mgeni Rasmi Simba Sc Vs Janweng

Klabu ya Simba sc kupitia kwa meneja wa Idara ya habari ya klabu hiyo Ahmed Ally imetangaza kuwa beki wa klabu hiyo raia wa DR Congo Henock Inonga atakua mgeni rasmi katika mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Janweng Galaxy utakaofanyika siku ya Jumamosi Machi 2 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Inonga amepewa heshima hiyo ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake kuifikisha timu yake ya Taifa ya Congo hatua ya nusu fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika (Afcon 2023) yaliyomalizika nchini Ivory Coast ambapo beki huyo alicheza zaidi ya asilimia tisini ya michezo hiyo.

“Mgeni rasmi katika mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy ni Henock Inonga sababu ndio mchezaji pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ameifikisha timu yake ya taifa kwenye nafasi ya nne kwenye AFCON 2023.” Alisema Ahmed Ally wakati akizungumza na waandishi wa habari mchana wa leo akizungumzia maandalizi kuelekea mchezo huo.

Pia Ahmed aligusia kuhusu timu za Tanzania kufuzu hatua ya robo fainali ikiwemo Yanga sc ambayo imefuzu kwa kuifunga Cr Belouzdad kwa mabao 4-0 ambapo alisema kuwa anayepaswa kushukuriwa ni muwekezaji wa klabu hiyo Mohamed Dewji kwa uwekezaji uliotukuka kiasi cha kuwaamsha wawekezaji wengine.

“Kufuzu kwa Yanga SC katika hatua ya robo fainali wa kushukuriwa ni Rais wa heshima wa Simba ni Mohammed Dewji na wa pili ni Simba SC kwa maana wakati Mo anakuja kuwekeza Simba alisema vision yake ni kushinda ubingwa wa Afrika na baada ya hapo tukaanza mchakato wa kutawala soka la Afrika”.
Wakati Mohammed Dewji anatengeneza dira ya kutawala soka la Afrika vilabu vingine vilikuwa vimelala usingizi wa pono, vilikuwa haviwazi kushindana Afrika na kusumbua na sasa baada ya miaka mitano ndio na wengine wameamka na wenyewe kutaka kuanza kufanya vizuri. Kama Simba SC na Mohammed Dewji tungeendelea kulala basi hadi sasa hakuna klabu yoyote Tanzania ingekuwa na hasira, malengo ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika ndio maana nasema robo fainali yao ya kwanza wa kushukuriwa ni Mohammed Dewji ndio aliwaamsha watu kutoka kwenye usingizi. Huu ndio ukweli ambao utadumu milele.”Alisema Ahmed akizungumza kwa mbwembe.
Simba sc inakabiria na mchezo mgumu dhidi ya timu ya Janweng Galaxy kutoka nchini Botswana ambapo anapaswa kushinda mchezo huo ili kufuzu hatua ya robo fainali kama watani zao Yanga sc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka