Connect with us

Soka

Ijumaa Kujulikana Mbivu Mbichi

Baada ya klabu ya Yanga sc kutoka suluhu katika mchezo wake wa ligi ya mabingwa hatua ya nusu fainali dhidi ya Mamelod Sundowns ya Afrika ya kusini huku Simba sc ikikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa mabingwa mara ya tano wa michuano hiyo Al Ahly Fc ambapo hatma ya timu hizo kufuzu kwenda nusu fainali itajulikana siku ya Ijumaa April 5.

Siku hiyo ndipo michezo ya marudiano ya michuano hiyo itafanyika ambapo mapema saa tatu usiku Yanga sc itakua na kibarua kigumu cha kupambana na Mamelod Sundowns jijini Pretoria huku Simba sc ikijitupa uwanjani saa tano usiku jijini Cairo nchini Misri.

Kutokana na matokeo ya michezo ya awali katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam timu zote Simba sc na Yanga sc zitakua na wakati mgumu zaidi katika michezo hiyo kutokana na ukweli kwamba hazikupata ushindi nyumbani huku zikikutana na timu ngumu zaidi katika michuano hiyo ambapo pia zina uzoefu wa kutosha hasa katika hatua ya robo fainali.

Sababu nyingine ambayo imefanya kuwe na ugumu kwa timu hizo kupata matokeo ni ukweli kwamba vikosi vya timu zote hasa eneo la ushambuliaji limekua na changamoto ya matumizi ya nafasi ambapo Simba sc washambuliaji wake Kibu Dennis na Saido Ntibanzokiza walikosa nafasi za wazi katika mchezo wa kwanza huku Clement Mzize na Kennedy Musonda nao walikosa pia mabao ya wazi ambapo katika michuano hiyo ni ngumu kupata nafasi mara mbili ama zaidi hivyo nafasi moja inapaswa kutumika kisawasawa.

Pia pamoja na hayo klabu zote mbili kwa sasa zimekua na uzoefu katika michezo ya ugenini pamoja na kujua namna gani ya kuepuka fitna ndogondogo ambapo zimekua na historia ya kupata ushindi ugenini ikikumbukwa Yanga sc iliwahi kuifunga Usm Algers katika mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho huku pia ikizifunga timu kama Club Africaine,Tp Mazembe,Mallumo Gallants huku Simba sc ikiifunga Primera de Augusto 3-1 ugenini pamoja na ushindi wa 2-0 dhidi ya Nyasa Big Bullets ugenini nchini Malawi.

Simba sc na Yanga sc hazina budi kukimbia zaidi uwanjani kuliko wenyeji ili kufika maeneo mengi ya uwanja pamoja na kuongeza ufanisi hasa katika kukaba ili kuepuka na kadi nyekundu na faulo za karibu na goli ama penati huku wakijitahidi kuwaheshimu wapinzani badala ya kupishana nao uwanjani huku ikibidi kuupeleka mchezo hatua ya matuta ambapo bahati pia huamua wakati mwingine.

Tanzania tupo nyuma yenu watani wa jadi…Solidarity Forever..

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka