Connect with us

Soka

Ighalo Kumalizia Msimu United

Klabu ya Manchester United imefikia makubaliano na klabu ya Shangai Shenghua juu ya mchezaji Odian Ighalo ambaye atasalia klabuni hapo hadi julai 31 mwisho wa msimu wa ligi kuu nchini Uingereza.

Awali Staa huyo Raia wa Nigeria alisaini mkataba wa mkopo wa muda wa miezi sita uliokua unaisha Mei 31 lakini kusimamishwa kwa ligi kuu ya Uingereza kutokana na kusambaa kwa ugonjwa wa homa ya Mapafu unaosababishwa na Virusi vya Corona ambapo sasa itabidi ligi hiyo kumalizika julai.

Ighalo ameonekana kufurahia maisha klabuni hapo huku pia akifunga magoli manne katika mechi nane hali inayowafanya United kufikiria kumsajili jumla japo tayari klabu yake imemwekea mshahara wa Paundi laki 4 kwa wiki ili aongeze mkataba wa kubaki nchini China.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka