Connect with us

Makala

Hispania Yatwaa Euro 2024

Timu ya Taifa ya Hispania imefanikiwa kuchukua taji la michuano ya Euro 2024 iliyokua ikifanyika nchini Ujerumani baada ya kufanikiwa kuifunga England kwa mabao 2-1 katika fainali ya michuano hiyo iliyofanyika katika uwanja wa Olympia jijini Berlin,Ujerumani.

Hispania ambayo haijapoteza hata mchezo mmoja katika michuano hiyo ilionyesha dalili za kutwaa ubingwa huo mapema kuanzia mwanzo wa mchezo baada ya kuumilika mchezo kwa kiasi kikubwa huku Nico Williams akiwatanguliza na bao la mapema dakika ya 47 ya kipindi cha pili akimalizia pasi safi ya Lamine Yamal.

Bao hilo lilisawazishwa na Cole Palmer dakika ya 73 ikiwa ni muda mchache baada ya kuingia uwanjani lakini furaha haikudumu kwani zikisalia dakika nne mchezo kumalizika Mikel Oyalzabal alifunga bao la pili akipokea pasi safi ya Cucurella.

Mwamuzi wa kati baada ya dakika nne za nyongeza alimaliza mchezo na kuzua shangwe kwa Wahispania waliojaa uwanjani hapo ambapo pamoja na kombe pia mchezaji Rodri alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa michuano hiyo huku kinda Yamal akitwaa tuzo ya mchezaji bora kijana.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala