Connect with us

Soka

Hersi Aula Caf

Rais wa klabu ya Yanga sc Eng.Hersi Ally Said ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama cha klabu za soka barani Africa (ACA) katika mkutano wa uzinduzi wa chama hicho uliofanyika Novemba 30 jijini Cairo nchini Misri.

Mkutano huo ulihudhuriwa na mabosi wakubwa wa vilabu barani Afrika wakiongozwa na Rais wa Caf Patrice Motsepe ambapo baada ya kupiga kura Hersi ambaye ni Rais wa kwanza wa Yanga sc alichaguliwa baada ya kupata kura asilimia 99 ya wajumbe wa mkutano huo.

Katika nafasi hiyo Hersi anakua mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho  akisaidiwa na Jessica Motaung wa Kaizer Chiefs na Paul Basset wa Akwa United.

Moja ya malengo ya Chama cha ACA ni kulinda, kukuza na kuweka mazingira wezeshi kwa maslahi ya vilabu vya Afrika. Aliendekea kuwapa msisitizo wenyeviti na baadhi ya viongozi wa vilabu hivyo kuwa wanachama hai wa chama hicho.

Chama kitawakutanisha wadhamini, wawekezaji, sekta binafsi,Serikali na wadau mbalimbali ambao watakuwa na ushirikiano kwenye kuendeleza miundombinu ya vilabu yenye sifa na vigezo vya CAF na FIFA, hili ni jukwaa lingine la kuliweka soka la Afrika pamoja kupitia viongozi wake na mijadala mingine itafanyika.

Baada ya miezi kadhaa mchakato umekamilika na Dr.Motsepe aliwaagiza viongozi wa vilabu zaidi ya 60, kukutana tena Cairo kwaajili ya uzinduzi wa Chama hicho, hatimae kura zikapigwa Hersi ambaye ni  kipenzi cha wanayanga akapewa jukumu zito.

Dr. Motsepe wakati anazindua Chama hicho alisema. “Uundwaji wa Chama cha (ACA) ni sehemu muhimu ya kuongeza na kukuza mawasiliano na ushirikiano baina ya CAF na vilabu vya soka Afrika, The African Club is bright”.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka