Connect with us

Soka

Hazard kurejea Chelsea?

Nahodha wa timu ya Taifa ya Ubelgiji Eden Hazard huenda akapata nafasi nyingine ya kurudisha kiwango chake kilichozoeleka baada ya klabu yake ya zamani Chelsea kufikiria kumrudisha tena darajani.

Mchezaji huyo amekuwa kwenye kiwango duni tangu ajiunge na Real Madrid misimu miwili iliyopita na kwa muda mrefu amekuwa kwenye meza ya matibabu kutokana na majeraha ya mara kwa mara.

Chelsea wanaandaa mpango wa kumsajili upya Hazard ili akakiongezee nguvu kikosi hicho kilichokosa makali katika safu ya ushambuliaji kutokana na wachezaji wa eneo hilo kuwa na viwango vya kupanda na kushuka.

Real Madrid ina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Paris St German Kylian Mbappe kama mbadala wa Eden Hazard katika dirisha lijalo la usajili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka