Connect with us

Makala

Hamza Mbioni Kurejea Simba sc

Beki wa klabu ya Simba Sc Abdulrazak Hamza leo amefanyiwa vipimo vya afya kwa awamu ya pili ili kufahamu maendeleo ya majeraha yake yanayomsumbua ambayo yamesababisha akosekane mazoezini mwa klabu hiyo.

Hamza aliumia katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Dodoma Jiji ambapo Simba sc waliibuka na ushindi wa 1-0 na kisha akajitonesha tena walipocheza na Coastal Union hali iliyomfanya beki huyo kushindwa kujiunga na timu ya Taifa ya Tanzania iliyocheza dhidi ya Congo Dr siku ya jana.

Madaktari wa klabu ya Simba Sc leo wamemfanyia vipimo kuona kama jeraha hilo limepona kabisa ama anahitaji matibabu ya aina nyingine kabla ya kurejea mazoezini kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga sc utakaofanyika Oktoba 19.

Hamza amekua na wakati mzuri tangu asajiliwe na klabu ya Simba Sc ambapo amekua chaguo la kocha Fadlu Davis katika kikosi cha kwanza akicheza yeye na Che Malone Fondoh kama mabeki wa kati huku staa wa kimataifa Chamou Karabou akisubiri nje.

Mpaka sasa Simba sc imecheza michezo mitano ya ligi kuu ya Nbc nchini ikiwa katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu ikiwa na alama kumi na tatu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala