Connect with us

Soka

Hali Tete Yanga

Hali ya upepo imebadilika katika klabu ya Yanga baada ya kupata matokeo ya sare mfululizo katika mechi tatu za ligi kuu Tanzania bara.

Yanga ilianza kupata sare dhidi ya Mbeya city kisha ikatoa suluhu na Prisons na tena katika mchezo wake dhidi ya Polisi Tanzania ikatoa sare licha kuongoza kwa goli la Tariq Seif dakika ya 41.

Klabu hiyo inakabiliwa na hali tete baada ya kulazimika kwenda uwanja wa Mkwakwani Tanga kwenda kupambana na Coastal union ambaye imetoka kujeruhiwa kwa mabao 2-1 na Ruvu Shooting.

Pia Yanga itakua na wakati mgumu kupambana na timu hiyo inayonolewa na Juma Mgunda ambaye ni kocha mzoefu wa ligi kuu na michuano ya kimataifa akitoka kuifundisha Taifa Stars katika michuano ya chalenji.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka