Connect with us

Soka

Gwambina vs Yanga Moto Utawaka

Leo katika ligi kuu Tanzania bara klabu ya Yanga sc itavaana na Gwambina fc katika mchezo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua ambao utafanyika katika uwanja wa Gwambina Complex katika mji mdogo wa Misungwi jijini Mwanza.

Yanga itahitaji kumalizia ziara yake ya kanda ya ziwa kwa kuibuka na pointi zote tisa baada ya kuzifunga Kmc 2-1 na Biashara united 1-0 hivyo Gwambina itabidi wajipange sawasawa kuwakabili vijana wa Cedrik Kaze huku uwepo wa Mwinyi Zahera kama mkurugenzi wa ufundi katika klabu ya Gwambina ukitajwa kuwa na msisimko anapokutana na waajiri wake wa zamani.

Katika msimamo wa ligi Yanga wako nafasi ya pili wakiwa na alama 22 sawa na vinara Azam Fc huku Gwambina wakiwa nafasi ya 14 licha ya kucheza michezo tisa wamepata alama  9 pekee huku wakiwa wamefungwa mabao mengi kuliko waliyoshinda.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka