Connect with us

Soka

GSM waidhamini ligi kuu

Kampuni ya GSM wameingia mkataba wa miaka miaka miwili na shirikisho la soka nchini kupitia bodi ya ligi kudhamini ligi kuu soka Tanzania Bara wenye thamani ya Tsh bilioni 2.1.

Hafla ya utiaji saini mkataba imefanyika hii leo katika hoteli ya kitalii ya Serena jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM Injia Hersi Said ndiye aliyeiwakilisha kampuni hiyo katika tukio hilo huku kwa upande wa TFF lilisimamiwa na makamu wa rais Athumani Nyamlani.

                                           

Hatua hiyo ni katika harakati za bodi ya ligi kuongeza thamani ya ligi kuu kwa kuhakikisha ongezeko la wawekezaji ambao kwa nafasi zao watatatua changamoto mbalimbali zinazoikabili ligi hiyo.

GSM inaungana na kampuni ya Azam,Shirika la habari nchini TBC pamoja na benki ya NBC kama wadhamini rasmi wa ligi kuu inayoendelea.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka