Connect with us

Soka

Gsm Kujenga Uwanja wa Kaunda

Habari njema kwa mashabiki wa Yanga sc ni kwamba mdhamini na mfadhili wa klabu hiyo Ghalib Said Mohamed (GSM) ameridhia kushiriki kwenye ujenzi wa uwanja wa  Yanga unaotarajiwa kujengwa katika eneo la jangwani jijini Dar es salaam yalipo makao makuu ya klabu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Rais wa klabu hiyo Hersi Said iliyotolewa kwa umma wakati klabu hiyo ikiadhimisha miaka 89 ya tangu kuaanzishwa kwake,uamuzi huo wa GSM umekuja baada ya kufanyika mazungumzo ya muda mrefu.

“Nipende kuwataarifu wanachama na mashabiki wa klabu yetu kuwa leo, GSM ameridhia kwa dhati kushiriki kwenye kufanikisha ujenzi wa uwanja wa kisasa wa Young Africans” amesema Hersi katika taarifa yake aliyoitoa ikiwa ni salamu zake kwa Wananchi ambao leo wanatimiza miaka 89.Ilisomeka taarifa hiyo fupi.

Yanga sc wapo katika mkakati kabambe wa kujenga uwanja wao wenye uwezo wa kuingiza takribani watu elfu 20-30 katika eneo lao ambalo ulikuwepo uwanja wa Kaunda ambao ulikua unatumika kama uwanja wa mazoezi kwa klabu hiyo miaka ya zamani.

Tayari maombi ya klabu hiyo ya kuomba nyongeza ya eneo kwa mamlaka limekubali kutokana na mradi mkubwa wa uendelezaji wa bonde la mto msimbazi unaotekelezwa na benki ya dunia kushirikiana na Ofisi ya Rais Tamisemi ambao ndio wanaratibu huku zaidi ya bilioni 598 zitatumika katika hatua ya awali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka