Connect with us

Soka

Gerard kutua Aston Villa

Kocha wa Rangers FC ya Scotland Steven Gerard anatarajiwa kujiunga na klabu ya Aston Villa ndani ya masaa 48 yajayo kwa mujibu kutoka wa taarifa kutoka kituo cha michezo cha skysports cha Uingereza.

Makubaliano ya kiasi kati ya paundi milioni 3 hadi 5 za Kiingereza yamefikiwa kati ya Rangers na Aston Villa kusitisha mkataba wa Gerard na msaidizi wake Gary McAllister,pia makubaliano mengine yanaendelea kufikia kuhamishia benchi lake zima Villa Park.

Nahodha huyo wa zamani wa Liverpool atasaidi mkataba wa kuitumikia timu hiyo hadi mwaka 2024.

Gerard ameshinda vita hiyo ya kuchukua mikoba hiyo iliyoachwa wazi na Dean Smith aliyefukuzwa kazi,baada ya kuonesha nia ya dhati kurejea Uingereza kujipima zaidi kwenye ushindani mkubwa.

Kocha ameipa Rangers ubingwa wa Scotland msimu uliopita kwa mara ya kwanza baada ya misimu tisa na kumaliza utawala wa Celtic katika ligi hiyo ya Uskochi.

Kazi kubwa mbele yake ni kuiwezesha Villa kuanza kupata matokeo baada ya kucheza michezo mitano ya mwisho na kupoteza yote,licha ya klabu iyo kufanya usajili mzuri wa Leon Bailey,Buendia na Danny Ings.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka