Connect with us

Makala

Gamondi Bye Bye Yanga Sc

Sasa ni rasmi klabu ya Yanga sc imeachana na kocha wake mkuu Miguel Gamondi pamoja na msaidizi wake Mussa Ndaw kwa makubaliano ya pande mbili huku sababu kubwa ikitajwa ni nidhamu mbovu pamoja na kushindwa kuimarisha umoja ndani ya timu hiyo.

Gamondi ambaye alijiunga na Yanga Sc akichukua nafasi ya kocha Nasredine Nabi na kufanikiwa kuipatia klabu hiyo mataji matatu ya ligi kuu ya Nbc na kombe la Shirikisho pamoja na Ngao ya Jamii msimu huu.

Licha ya kwamba kocha huyo alisaini mkataba mpya wa mwaka mmoja mwanzoni mwa msimu huu lakini kupata matokeo mabaya katika michezo miwili dhidi ya Azam Fc na Tabora United huku mastaa wa klabu hiyo wakionyesha viwango vibovu imesababisha mabosi hao kufikia hatua ya kumtema.

Pamoja na Gamondi pia baadhi ya watumishi wa klabu hiyo upande wa utawala nao wapo mbioni kuondolewa klabuni hapo ili kuunda safu mpya kuanzia ndani mpaka nje ya uwanja.

Gamondi atakumbukwa na mashabiki wa klabu ya Yanga sc kutokana na kufanikiwa kuipa kipigo cha mabao 5-1 watani wa jadi Simba sc huku pia akifanikiwa kuwafunga mara kadhaa katika michuano ya ligi kuu na Ngao ya jamii.

Kushuka kiwango kwa mastaa kama Stephane Aziz ki kunatajwa kuwa ni kutokana na kocha huyo kuruhusu mastaa hao kutokea nyumbani kila siku mazoezini ambapo huingia kambini siku moja kabla ya mechi kisha kurudi nyumbani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala