Connect with us

Makala

Gamondi Awapa Mbinu Mastaa Kuiua Cbe

Kocha wa klabu ya Yanga sc Miguel Gamondi amesema kuwa tayari amewapa mbinu mbalimbali mastaa wa klabu hiyo kuelekea mchezo wa marudiano wa hatua ya pili ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Cbe SA ya nchini Ethiopia.

Mchezo huo utakaofanyika kesho usiku katika uwanja wa Amaani Visiwani Zanzibar ambapo Yanga sc itaingia na mtaji wa bao moja ilioupata nchini Ethiopia katika mchezo wa awali.

Gamondi amesema kuwa amewapa mbinu mbalimbali mastaa wa klabu hiyo ili kuibuka na ushindi wa mabao mengi.

“Hali ya wachezaji wangu ni nzuri, tumejiandaa vizuri sana na tumepata muda wa kujiandaa. Nina wachezaji wakubwa sana ambao wanaweza kufanya jambo bora kuliko wapinzani wetu, najua wachezaji wangu wanafahamu umuhimu wa kufuzu hatua ya makundi”.Alisema Gamondi mbele ya waandishi wa habari.

“Mechi iliyopita kweli tulikosa nafasi nyingi. Lakini kama kocha kukosa nafasi hutokea, muhimu ni kuwa na timu yenye uwezo wa kutengeneza nafasi nyingi. Ukweli ni kwamba lazima kesho tutumie nafasi tunazopata. Sitaki kuwapa wachezaji wangu presha kisa tulikosa nafasi nyingi, najua watacheza kwa utulivu lakini muhimu ni kuhakikisha tunatumia nafasi tunazopata”alimalizia kusema kocha huyo aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja kusalia klabuni hapo.

Kwa upande wa mastaa wa klabu hiyo waliowakilishwa na Ibrahim Hamad walisema kuwa wao wamejiandaa kikamilifu kuelekea mchezo huo.

“Tunamshukuru Mungu asilimia kubwa wachezaji wote tupo salama. leo tunafanya mazoezi ya mwisho ni matumaini yetu tutamaliza salama, nina furaha kubwa sana mchezo huu kufanyika hapa Zanzibar nami nina matumaini makubwa kwenye mchezo huo”.Alisema beki huyo maarufu kwa jina la Bacca.

Yanga sc katika mchezo huo inapaswa kutoa sare ama kushinda kwa mabao yeyote ili kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo ya klabu bingwa barani Afrika kwa mara ya pili mfululizo ndani ya miaka miwili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala