Connect with us

Soka

Galaxy Waifanyia Mbaya Simba Sc

Klabu ya Janweng Galaxy ya nchini Botswana imeifanyia figisu klabu ya Simba sc baada ya kuamua kuhamisha mchezo baina ya timu hizo utakaofanyika siku ya jumamosi Disemba 2 mwaka huu kutoka uwanja wa Taifa wa Botswana kwenda uwanja wa Obedi Itani Chilume uliopo katika mji wa Francistown.

Mabadiliko ya mchezo huo yatawaathiri Simba sc ambao wanahitaji ushindi katika mchezo huo kutokana na sababu kuwa watalazimika kusafiri umbali wa kilomita mia nne kutoka mjini Gaborone mpaka mji huo wa Francistown ambapo usafiri wake ni wa basi ama ndege ambayo huchukua muda wa saa moja na dakika kumi.

Hata hivyo uamuzi wa kuhamisha uwanja umetolewa na shirikisho la soka barani Afrika(Caf) kutokana na uwanja wa Taifa wa nchi hiyo kutokidhi vigezo hivyo klabu hiyo kuamua kutumia uwanja huo ulioko mbali na mjini.

Klabu ya Simba sc inatarajiwa kuanza safari siku ya ijumaa kuelekea nchini humo huku tayari ikiwa imemtambulisha kocha mpya Abelhad Benchika ambaye amewasili na makocha wasaidizi wawili.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka