Connect with us

Soka

Feisal,Bruno Watwaa Tuzo Novemba

Bodi ya ligi kuu nchini Tanzania kupitia kamati maalumu ya usimamizi wa ligi imemtangaza mchezaji Feisal Salum kuwa mchezaji bora wa mwezi novemba akiwashinda Kipre Jn wa Azam Fc na Max Nzengeli wa Yanga sc ambao aliingia nao fainali.

Taarifa iliyotolewa na bodi hiyo imesema kuwa Feisal kwa mwezi huo aliisaidia Azam fc kupata ushindi akifunga mabao mawili na kusaidia upatikani wa mengine manne katika michezo mitatu ambapo alicheza jumla ya dakika 254.

Pia kwa upande wa mwingine kocha wa klabu hiyo Bruno Ferry naye amefanikiwa kutwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi huo huo wa Novemba akiwashinda Miguel Gamondi wa Yanga sc na Heron Ricardo wa Singida Big Stars.

Bruno aliiongoza klabu yake kushinda michezo mitatu dhidi ya Mashujaa Fc 3-0,Ihefu Fc 3-1 na Mtibwa Sugar 5-0 na kuifanya klabu hiyo kupata alama zote tisa katika michezo hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka