Taarifa za ndani zinasema kuwa kiungonwa Azam Fc Feisal Salum atakutana na viongozi wa klabu hiyo kujadili mkataba mpya siku ya ijumaa atakaporejea Dar Es Salaam baada ya mchezo wa ligi kuu ya Nbc dhidi ya Namungo FC pale Ruangwa.
Inaelezwa Feisal Salum hayupo tayari kuongeza mkataba mwingine na Azam FC kwa sasa lakini anaweza kufikiria kusalia klabuni hapo kama atalipwa mshahara wa shilingi millioni 70 kwa mwezi ili kupita kiwango anacholipwa mshambuliaji raia wa Colombia Jhonier Blanco ambae analipwa millioni 50.
Hadi sasa Klabu ya Simba inaongoza kuwa na mahitaji makubwa na Feisal Salum na tayari kuna mawasiliano yanaendelea na wawakilishi wa mchezaji huyo ambapo Simba sc inatamani kumsajili Feisal Salum dirisha dogo na ikishindikana dirisha kubwa la usajili.
Hata hivyo mabosi wa Simba sc wakiongozwa na Tajiri Mohammed Dewji pamoja na kuwa na pesa za kutosha inabidi wapambane haswa kutokana na mkataba baina ya Azam Fc na Yanga sc kuweka vipengele vigumu wakati wa mauziano ya mchezaji huyo.
Pia ugumu mwingine unakuja kutokana na Azam Fc inamuhitaji staa huyo asalie klabuni hapo huku Yanga sc pia ikimhitaji kumrudisha klabuni hapo kwa mara ya pili hasa pindi atakapoondoka Stephan Aziz Ki ambaye mpaka sasa analipwa pesa nyingi klabuni hapo baada ya kusaini mkataba mpya.