Connect with us

Soka

Feisal Aizamisha Yanga sc

Klabu ya Azam Fc imefanikiwa kuchukua alama tatu katika mchezo wa ligi kuu ya soka ya Nbc nchini baada ya kuifunga Yanga sc kwa mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Yanga sc ambayo ilimkosa Khalid Aucho ambaye ni majeruhi ilianza kupata bao la mapema dakika ya 10 kupitia kwa Clement Mzize ambaye alipata pasi nzuri kupitia kwa Stephan Aziz Ki ambapo bao hilo lilisawazishwa na Gibril Sillah dakika ya 19 kutokana na mabeki wa Yanga sc kushindwa kuondoa hatari mapema.

Mzize alipata takribani nafasi tano lakini alishindwa kufunga huku kuumia kwa Pacome Zouzou kulisababisha Yanga sc kupotea eneo la katikati baada ya kuingia Joseph Guede ambaye alishindwa kuendana na kasi ya mchezo dhidi ya viungo hatari wa Azam Fc wakiongozwa na Yahya Zayd.

Feisal Salum alizamisha jahazi la Yanga sc kwa shuti kali dakika ya 51 bao ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo licha ya jitihada ya Yanga sc kusawazisha bao hilo ambapo juhudi hizo zilikwama kutokana na Azam Fc kujaza viungo wengi eneo la katikati.

Azam Fc sasa imefikisha alama 47 dhidi ya 52 za Yanga sc ambao wapo kileleni lakini wakiwa na mchezo mmoja mkononi ambapo wakishinda dhidi ya Singida Big Stars watakua wameongeza pengo la alama mpaka nane huku Simba sc wakiwa nafasi ya tatu na alama 45 huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka