Connect with us

Soka

Fedha za Waarabu Zamvuta Okwi

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda(The cranes) Emmanuel Okwi yupo mbioni kukamilisha uhamisho wa kujiunga na timu inashiriki ligi kuu ya uarabuni (UAE) Fujairah Fc.

Okwi mpaka sasa ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na Simba sc na sasa anaruhusiwa kujiunga na klabu yeyote huku akiwa na ofa lukuki baada ya kufanya vizuri katika michuano ya Afcon baada ya kuifungia timu yake mabao mawili huku akiibuka mchezaji bora wa mechi (man 0f the match) mara moja dhidi ya kongo.

Kiwango chake kilizivutia timu kutoka Misri,Tunisia,Afrika kusini na Uarabuni,Taarifa zinadai uhamisho huo umekamilika kwa zaidi ya asilimia 80 ukisimamiwa na kampuni ya uwakala ya Seefaleslam Beleed ya nchini Misri.

Fujairah ni timu iliyoanzishwa mwaka 1968 na inashiriki ligi kuu ya uarabuni huku ikifanikiwa kuchukua kombe mara tatu japo msimu ulioisha ilimaliza nafasi ya 12 katika ligi yenye timu 14.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka