Connect with us

Soka

Fedha za Bruno Fernandes Zazua Kizaazaa

Klabu ya Sampdoria inayoshiriki ligi kuu ya Serie nchini Italia imefikisha malalamiko katika Shirikisho la soka Duniani(Fifa) kudai mgao wake katika mauzo ya mchezaji Bruno Fernandes kwenda Manchester United.

Awali staa huyo alikua mali ya Sampdoria ambapo aliuzwa mwaka 2017 kwq dau la Euro milioni 7 pamoja na nyongeza kadhaa huku kukiwa na kipengele cha kupata mgawo endapo staa huyo atauzwa kwenda klabu nyingine.

Januari Mwaka huu staa huyo amekamilisha uhamisho wake kwenda Manchester United kwa dau la paundi milioni 47 ambapo dau hilo litapanda mpaka paundi milioni 66 huku Sporting wakitakiwa kuwapo Sampdoria asilimia ya dau hilo lakini mpaka sasa hawajalipa.

Inadaiwa klabu hiyo inatakiwa kupewa kiasi cha paundi milioni 4 na Sporting Lisbon hali iliyowafanya kuripoti Fifa huku Sporting wakidau kuwa kipengele hicho kilikufa pindi walipomuongezea mkataba staa huyo mwaka 2018.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka