Connect with us

Soka

Farid Mussa Afunguka Kutopata Nafasi

Kiungo wa klabu ya Yanga sc Farid Mussa amefunguka kutoonekana kwake uwanjani tangu acheze katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ambapo Yanga sc ilipata ushindi wa mabao 5-0.

Farid amebainisha kwamba kupotea kwake uwanjani kumetokana na kuwa na majeraha ambaye yalimfanya akae pembeni na tangu apone sasa anajitahidi kufanya mazoezi kwa kasi ili kumshawishi mwalimu Miguel Gamondi ampe nafasi kikosini.

“Nilikuwa majeruhi, ila nimerudi naendelea na maandalizi kama kawaida, suala la kucheza namwachia Kocha Gamondi, mimi napambana kuhakikisha namshawishi ili aweze kunipa nafasi ya kucheza,”amesema Farid ambaye aliwahi kucheza Ulaya.

“Sijakata tamaa nitapambana kuhakikisha napata nafasi ya kucheza ili kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wameipa mafanikio timu japo sio rahisi lakini inawezekana”Alisema

Farid alikua ni mchezaji wa kutumainiwa kipindi anacheza Azam Fc kisha akaenda nchini Hispania na akarejea nchini na kujiunga na Yanga sc ambapo amedumu kikosini humo kwa takribani misimu mitatu sasa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka