Connect with us

Soka

Edwards kuondoka Liverpool

Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Liverpool Michael Edwards amethibitisha kuwa ni kweli ataondoka katika klabu hiyo mkataba wake utakapofikia tamati mwishoni mwa msimu wa kimashindani 2021/2022.

Edwards alijiunga na Liverpool mwaka 2011 na ndiye mtu aliyeleta mabadiliko na mafanikio makubwa katika idara ya usajili kwa misimu ya hivi karibuni.

Nafasi yake ya ukurugenzi wa michezo wa Liverpool itachukuliwa na msaidizi wake Julian Ward,licha ya kushawishiwa vya kutosha na wamiliki wa klabu hiyo Fenway Sports Group lakini amekataa ombi hilo na kuamua kuondoka zake.

Katika barua yake ya wazi kwa mashabiki wa Liverpool Edwards amesema ”miaka kumi ni mingi sana kwa maisha ya mfanyakazi,kwenye mpira wa miguu hizo ni kama zama hasa kwa klabu ya Liverpool ambapo matarajio siku zote huwa ni ya viwango vya juu na si vinginevyo.kuwa sehemu ya klabu hii ni kitu cha kujivunia kutokana na watu niliofanya nao kazi na mafanikio tuliyoyapata pamoja.

”Nilijiwekea kufanya kazi kwa miaka kumi pekee hapa,imefika kwangu inatosha japo ni ngumu kufanya uamuzi mgumu kama huu hasa kwa nyakati hizi ambazo tumerudi kwenye ubora wetu,katika wakati wangu tumefanya na kubadilisha mengi hivyo ni wakati sahihi kwa mtu mwingine kuleta kitu kipya kwenye klabu”.

Michael Edwards hana mpango wa kwenda kufanya kazi katika klabu ya Newcastle United licha ya wamiliki matajiri wa Saudi Arabia kutafuta mtu mwenye uzoefu mkubwa kwenye eneo hilo.

Mkurugezi huyo wa michezo atakumbukwa kwa kufanya sajili kubwa zilizoirudisha timu hiyo kwenye ubora wake kama wa kocha Jurgen Klopp,wachezaji kama Van Djik,Fabinho,Alisson Becker,Salah,Mane,Firmino,Matip na Joe Gomez tena kwa staili ya kimya kimya bila makelele wala uvumi wa muda mrefu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka