Mshambuliaji wa klabu ya Azam Fc Prince Dube amewasilisha barua ya kuomba kuvunja mkataba na klabu hiyo kutokana na kutokua na furaha ambapo ana mkataba na klabu hiyo mpaka mwaka 2026.
Dube aliyejiunga na Azam Fc msimu wa mwaka 2020 aliongeza mkataba wa miaka mitatu kusalia klabuni hapo mwanzoni mwa msimu uliopita na hivyo kumfanya kuwepo Chamazi mpaka mwaka 2026 na sasa anaomba kuuvunja mkataba huo alioutumikia kwa miezi sita pekee na kusalia na miaka miwili na nusu.
Mkuu wa Idara ya Habari ya klabu ya Azam Fc Zakaria Thabit amethibitisha kuwa mshambuliaji huyo amewasilisha ombi la kuvunja mkataba huku akijibu kuwa msimamo wa klabu hiyo ni kuwa alipe fedha ya kuvunja mkataba kiasi cha dola laki tatu za marekani ama kama kuna timu inamhitaji basi iwasilishe ofa mezani na kama hayo yatashindikana basi abaki kuutumikia mkataba wake.
“yuko huru kwenda anakotaka lakini anapaswa kulipa kiasi cha dola za kimarekani laki tatu ama abaki kuutimikia mkataba wake ambao umebaki miaka miwili na nusu”Alisema Zakaria
Taarifa za ndani zinasema kuwa staa huyo haelewani na kocha Yousouph Dabo huku akidai kuwa viongozi wa klabu hiyo wanamchukulia poa kwa kuwa amekaa klabuni hapo muda mrefu huku pamoja na jitihada za wachezaji wenzake kumtaka abaki lakini mpaka sasa Dube hayuko kambini na timu hiyo.
Dube amekuwa na kiwango bora sana japo mara nyingi amekuwa akikumbwa na majeraha ya mara kwa mara jambo ambalo pia linatokea kuathiri kiwango cha nyota huyo raia wa Zimbabwe ambapo katika msimu yake minne amkua akifunga mabao akianza na 2020/21 Goli 14,2021/22 Goli 1,2022/23 Goli 12 na 2023/24 Goli 7 ambapo jumla amefunga magoli 34 kwenye misimu minne ambayo ameitumikia klabu ya Azama Fc.