Connect with us

Makala

Dube Afungua Akaunti ya Mabao

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Prince Dube amefungua rasmi akaunti ya kufunga mabao klabuni hapo akiisaidia klabu yake ya Yanga sc kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya timu ya Ts Galaxy inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika ya kusini katika mchezo wa kirafiki wa maandalizi ya msimu mpya nchini Afrika Kusini.

Yanga sc ilianza na kikosi kilichotafasiriwa kama kikosi cha pili ambacho hakikua na mastaa wale waliozoeleka kuwa huwa wanaanza mara kwa mara wakiongozwa na Kipa Aboutwalib Mshery,Kibwana Shomari,Farid Musa,Dickson Job,Aziz Andambwile,Jonas Mkude,Mudathir Yahya,Salum Abubakar,Clement Mzize,Dennis Nkane na Shekhan Ibrahim.

Miguel Gamond alidhamiria kila mchezaji acheze mchezo huo ambapo pamoja na Yanga sc kuonekana kuelemewa kwa kushambuliwa mara kwa mara aliamua kumuingiza Jean Baleke na kipa Aboubakary Khomeiny kumalizia dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili kilianza matokeo yakiwa ni suluhu ambapo mastaa wote waliozolekwa wakiwa kipa Djigui Diarra,Yao Kouasi,Nickson Kibabage,Bakari Mwamnyeto,Ibrahim Bacca,Khalid Aucho,Duke Abuya,Max Nzengeli,Cletous Chama,Prince Dube na Stephane Aziz Ki waliingia na kuwafanya Galaxy watumie muda mwingi kuzuia baada ya kushambuliwa mara kwa mara.

Dube alifunga bao kwa shuti kali dakika ya 55 baada ya kupokea pasi mpenyezo kutoka kwa Stephane Aziz Ki na kupiga shuti kali lililomshinda kipa wa Ts Galaxy na bao hilo lilidumu mpaka dakika 90 za mchezo huo huku wenyeji wakikosa penati dakika za mwishoni mwa mchezo.

Yanga sc inatarajiwa kurudi uwanjani siku ya jumapili Julai 28 kukipiga na Kaizer Chiefs katika mchezo wa kirafiki wa mwisho kabla ya kumaliza maandalizi ya msimu na kurejea nchini kwa ajili ya Tamasha la Yanga day August 4 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala