Connect with us

Soka

Diarra,Mayele Kuwania Tuzo Afrika

Mshambuliaji Pyramids FC, Fiston Mayele na Mlinda Mlango wa Yanga Sc, Djigui Diarra ni sehemu ya wachezaji 20 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mashindano ya klabu kwa mwaka 2023.


Diarra yupo kwenye tuzo mbili katika tuzo hizo ambapo tuzo ya mchezaji bora wa kiume barani Afrika huku anawania pia tuzo ya Golikipa Bora Afrika akishindana na makipa Mohamed El Shenawy (Misri),Yassin Bounou (Morroco),Andre Onana (Cameroon),Ronwen Williams (Afrika kusini),Eduardo Mendy (Senegal),Oussama Benbout (Algeria),Youseff El Moutie (Morroco),Pape Mamadou SY(Morroco) na Landing Badji(Senegal).

Kwa upande wa Fiston Mayele na yeye yumo katika orodha ya  wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa Wanaume kwa wachezaji wanaocheza soka barani Afrika ambapo mastaa wengi kama Djigui Diarra,Makabi Lilepo,Percy Tau,Ranga Chivaviro na wengine ambao wamejitokeza katika orodha ya kipa bora hapo juu wameingia pia katika tuzo hii.

Kuorodheshwa huko kwa mastaa hao wa Yanga sc kumetokana na klabu hiyo kuwa na msimu mzuri wa 2022/2023 ambapo ilitwaa mataji yote ya ndani na kisha ikafika fainali za michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika ambapo ilikosa kombe kwa Usm Algers kwa bao la ugenini.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa katika hafla maalumu itakayofanyika nchini Morroco siku ya tarehe 11/12/2023 ambapo mastaa hawa wote wanapaswa kuhudhuria.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka