Connect with us

Soka

Diarra Arejea Yanga sc

Kipa namba moja wa klabu ya Yanga Sc raia wa Mali, Djigui Diarra amerejea nchini sambamba na kuingia kambini mapema ya leo  akitokea Katika majukumu ya timu ya taifa ya Mali iliyokuwa inashiriki Kombe la Mataifa Afrika (Afcon).

Diarra na timu yake ya Taifa walitolewa katika hatua ya robo fainali baada ya kufungwa 2-1 na wenyeji Ivory Coast ambapo kipa huyo alionyesha kiwango kikubwa katika michuano hiyo akiwa kama kipa namba moja wa timu ya Taifa.

Kurejea kwa kipa huyo kutaiboresha safu ya golini inayochezwa na Abdutwalib Mshery na Metacha Mnata anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara waliocheza dhidi ya Tanzania Prisons.

Kipa huyo mpaka sasa amepata cleansheet tano katika michezo aliyocheza ya ligi kuu nchini Tanzania kabla ya kusimama na kwenda kujiunga na timu ya Taifa ya Mali kwa ajili ya michuano ya Afcon 2024.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka