Connect with us

Soka

CONTE kutua SPURS

Kocha wa zamani wa vilabu vya Juventus,Chelsea na Inter Milan Antonio Conte amefikia makubaliano ya msingi na klabu ya Tottenham Hotspurs kuwa mkufunzi wa timum hiyo ya Kaskazini mwa London.

Conte atasaini mkataba na klabu hiyo leo Jumanne utakaomuweka Spurs hadi mwaka 2023.

Mkurugenzi wa michezo Fabio Paratici alimhitaji Conte tangu mwezi Julai lakini walishindwana dakika za mwisho na kutua kwa Mreno Nuno Santo ambaye amefutwa kazi.

Muitaliano huyo sio muumini wa kuchukua timu katikati ya msimu na alikuwa tayari kubadili mawazo yake alipokaribia kupata ofa ya Man Utd kabla ya kuamua kubakia na kocha wao Ole Solskjaer.

Conte alishawahi kufanya kazi na Fabio Paratici katika klabu ya Juventus na ndiye aliyemshawishi kuukubali mradi wa Totenham,kocha huyo amehakikishiwa kupewa sapoti katika madirisha yajayo ya usajili kukiboresha kikosi hicho.

Ujio wa mkufunzi huyo mshindi wa mataji mbalimbali huenda ukamshawishi nahodha wa klabu hiyo Harry Kane kusalia kwenye timu hiyo.conte

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka