Connect with us

Soka

Comoro Yatolewa Kibabe

Timu ya taifa ya Comoro imetolewa katika michuano ya Afcon 2022 nchini Cameroon baada ya kukubali kichapo cha mbao 2-1 kutoka kwa wenyeji Cameroon licha ya Comoro kucheza kwa muda mrefu wakiwa pungufu katika mchezo huo mkali uliosisimua mashabiki wengi wa soka duniani.

Comoro ambao idadi kubwa ya wachrzaji wake walikutwa na ugonjwa wa Corona na kusababisha wasicheze mchezo huo akiwemo kocha mkuu pamoja na mastaa zaidi ya saba hali iliyowalazimu kumtumia beki wa pembeni Chaker Alhadhur kama kipa katika mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Olembe jijini Yaoundé.

Karl Toko Ekambi alifunga bao dakika ya 29 na kuwapa wenyeji uongozi huku wakilazimika kucheza pungufu baada ya dakika ya 7 ya mchezo mchezaji wa Comoro Nadjim Abdou baada ya kumchezea faulo Moumi Ngamaleu.

Licha ya kuwa pungufu Comoro walishambulia lango la Cameroon na kumlazimisha kipa Andre Onana anayechezea klabu ya Ajax kufanya kazi ya ziada kuokoa hatari langoni mwao huku wenyeji wakipata bao la pili dakika ya 70 Vincent Aboubakar huku Comoro wakichomoa dakika ya 81 kupitia mkwaju wa faulo wa nahodha Youssouf M’Changama.

Cameroon wanaungana na Gambia kwenda hatua ya robo fainali huku mpaka sasa wenyeji wakipewa nafasi kubwa ya kunyakua kombe hilo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka