Connect with us

Soka

Chama,Miqquison Waikosa Azam Fc

Mastaa Cletous Chama,Luis Miqquison na Saido Ntibanzokiza wataukosa mchezo wa ligi kuu dhidi ya klabu ya Azam Fc utakaochezwa leo Mei 9 katika uwanja wa Benjamin Mkapa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo adhabu na majeraha.

Kikosi cha Simba sc kinachoshuka uwanjani katika mchezo huo kimetangazwa huku mastaa hao sambamba na Henock Inonga Baka wakiwa hawapo ambapo inafahamika kuwa Chama anatumikia adhabu ya kufungiwa na mamlaka za soka michezo mitatu huku Saido na Luis Miqquison wakisumbuliwa na majeraha.

Simba sc inashuka dimbani dhidi ya Azam Fc kutafuta alama tatu muhimu ambazo zitaipa faida ya kumaliza nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu nchini ambapo endapo itafanikiwa kuifunga Azam Fc katika mchezo huo itapunguza alama tatu zaidi na kuweka mazingira mazuri ya nafasi hiyo maana Yanga sc mpaka sasa ina asilimia tisini kuchukua ubingwa wa ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka