Connect with us

Soka

Cantona akosoa kombe la dunia

Gwiji wa soka wa zamani wa Manchester united Eric Cantona ameoneshwa kukerwa na michuano ya kombe la dunia zitakazofanyika mwaka huu nchini Qatar  huku akiweka wazi kuwa hatajisumbua kuitazama.

Cantona ameyasem hayo alipokuwa kwenye mahojiano na gazeti la Independent la Uingereza.Alisema kuwa ”sielewi kwanini Qatar imechaguliwa kuandaa mashindano haya,Qatar siyo nchi ya soka,Marekani ni nzuri kwani kuna msukumo mkubwa kwa soka la wanawake hivyo lingefaa kwenda kwani lingesaidia zaidi ukuaji wa soka.

Hakuna ukuaji wa soka wa namna hiyo Qatar.Utaona ni kwa sababu za kifedha tu zimesababisha fainali zipelekwe huko,watu wengi wamekufa wakati wa uandaaji wa mashindao hayo.

Aliendelea sijali,sitayaangalia kwakweli,siyo kombe la dunia kwangu binafsi,maisha ya watu yameharibiwa na bado sisi wengine tufurahie mashindano?haiwezekani”.

Kauli ya gwiji huyo huenda ikazua mijadala mbalimbali duniani hususani juu ya uhalali wa Qatar kupewa haki hiyo ya kuandaa ukizingatia ukandamizaji mkubwa wa haki za kibinadamu na sheria kali dhidi ya jinsia ya kike.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka